Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, ameongoza wafanyakazi wa BoT kushiriki katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2025 zilizofanyika leo, tarehe 27 Julai 2025, jijini Dodoma.
Katika mbio hizo zilizowakutanisha washiriki kutoka sekta mbalimbali, wafanyakazi wa BoT walishiriki katika makundi tofauti ya mbio, ikiwemo kilomita 5, 10, 21 na 42.
Ushiriki wa Benki Kuu katika mbio hizo unaonyesha dhamira ya BoT si tu katika masuala ya uchumi na fedha, bali pia katika kuwekeza kwenye afya ya rasilimali watu wake na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kijamii.