Wachezaji wa Mpira wa miguu Kikosi cha Mgera Fc wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa Mpira wa miguu Kikosi cha Kalenga F wakiwa katika picha ya pamoja.
……..
TIMU ya Soka ya Mgera fc imefanikiwa kutinga fainali ya mashindano ya kombe la Vunjabei baada ya kuibonda Kalenga fc katika hatua ya mikwaju ya penati 5 – 3.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye viwanja vya Shule ya msingi Mlandege hadi dakika 90 zilishindwa kutambiana.
Baada ya filimbi ya mwisho ndipo hatua ya matuta ikaamua nani wa kwenda Fainali ambapo katika mchezo huo Kalenga fc watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi walizopata.
Kutokana na kuingia fainali timu ya Mgera Fc imejihakilishia kuondoka na kitita cha mshindi wa pili endapo watashindwa kuibuka mabingwa.
Mchezo wa pili wa nusu fainali utachezwa Julai 29 ambapo BBC Fc wanaopewa nafasi kubwa kuibuka na ubingwa wataumana na Kisinga Fc .
Ikumbukwe kuwa mashindano hayo bingwa ataibuka na kitita cha milioni 10 ambapo inadhaminiwa na kampuni ya Vunjabei.