Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma M. Rajab amefanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Oman, Prof. Mahad Said Ali Baawain, yalifanyika katika Ofisi za Wizara hiyo Julai 08, 2025
Wawili hao pamoja na mambo mengine walijadiliana namna ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Oman.
Balozi Fatma alieleza kuwa moja ya eneo ambalo Tanzania na Oman zinashirikiana ni sekta ya kazi na ajira na kusisitiza ili uhusiano huo uendelee kunawili na kuwa na manufaa kwa pande zote mbili, kuna umuhimu wa kuharakisha Rasimu ya Makubaliano ya Kazi na Ajira ili iweze kusainiwa hivi karibuni.
Balozi Fatma alisema Tanzania ni moja ya nchi zinazopeleka kiasi kikubwa cha wafanyakazi nchini Oman na
ili iweze kuendelea kufaidika na soko la Ajira katika sekta mbalimbali, ni muhimu makubaliano hayo yakamilike na kusainiwa.