Mabondia Kassim Mbundwike na Mwanjango wameshinda mapambano yao katika michuano ya maadhimisho ya miaka 50 ya Sherehe za Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro iliyoshirikisha mabondia toka Madagascar,Gabon,Tanzania na wenyeji Comoro.
Mabondia hao wamewasilisha vikombe vyao kwa Balozi wa Tanzania nchini humo,Saidi Yakubu kwa uratibu wa mwambata jeshi,Abdulrahim Mahmoud Abdallah.Balozi Yakubu aliwapongeza kwa ushindi huo ambao umefungua ukurasa mpya wa diplomasia ya michezo.
Michuano hiyo ilihudhuriwa na Rais wa Umoja wa Visiwa hivyo,Azali Assoumani.