KAMPUNI ya Lake Energy Tanzania imeiomba Serikali kuwadhibiti wafanyabiashara wanaingiza kiwango kikubwa cha Nondo nchini Tanzania kutoka Mataifa ya nje huku wakiuza Nondo hizo kwa bei ya chini hali ambayo inasababisha kampuni hiyo kukosa soko jambo ambalo linaondoa hali ya ushindani wa kibiashara
Witohuo umetolewa hii leo Jijini Dar es Salaam na Bwana Ally Swaleh Mbarak, Afisa masoko wa bidhaa za Viwandani kutoka Kampuni ya Lake Energy wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Monyesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba kuusiana na punguzo la bidhaa zinazouzwa na kampuni hiyo wakati wa Msimu wa sabasaba na kubainisha kuwa, kiwango kikubwa cha Nondo kinachoingizwa nchini kinaathiri soko ya ndani
Naye Ally Mngazija ambae ni Afisa mauzo wa bidhaa za Vilainishi vya Magari kutoka Lake Energies amebainisha namna ambavyo kampuni hiyo hulazimika kubadili muundo wa vifungashio vya bidhaa zao za ili kupambana na vitendo vya uchakachuaji wa bidhaa hizo kwalengo la kuhakikisha wateja wao wanapata bidhaa zilizo bora na halisi kutoka Lake Energy
Aidha Edwin Christopher ambae ni Afisa Masoko kutoka Lake Enegy amesema kuwa Katika Kuunga mkono Jitihada za Serikali kuhusu nishati safi ya kupikia Lake Energy kwakushirikiana na REA wamefanikiwa kusambaza mitungi ya gesi zaidi ya Lakimoja na nusu (150,000) katika Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma, usambazaji uliofanywa kupitia vituo vya 150 vya Lake Energy vilivyopo maeneo mbalimbali kote nchini.
Lake Energy nikampuni inayojihusisha na uzalishaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani, mitungi ya gesi, vituo vya mafuta, vipuri vya magari, nondo na bidhaa nyingine mbalimbali