Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene (kushoto), baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene (kushoto), baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene (wa pili kushoto), baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu – Fedha na Uwekezaji kutoka UNDP, Emmanuel Nnko na kushoto ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIGF), Kennedy Mmassy.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nne kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene (wa nne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wizara ya Fedha na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESFR), baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Robert Mtengule, akiteta jambo na Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. John Shilinde, baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwa Katibu Mkuu wizarani hapo, Treasury Square, jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).
…………
Na. Farida Ramadhani, WF, Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi hiyo katika maendeleo ya nchi hususan katika masuala ya kiuchumi na kijamii.
Amekutana naye ofisini kwake jijini Dodoma, ambapo alimwelezea maeneo ya kipaumbele nchini yanaongozwa kwa muda mrefu na Dira ya Maendeleo ya Taifa, kwa muda wa kati kupitia Mipango ya Maendeleo ya Miaka Mitano, na kwa muda mfupi kupitia Mpango wa Maendeleo wa kila Mwaka.
Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kuongeza nafasi za ajira, kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya umaskini, na kuongeza mauzo ya nje na hivyo kuchangia kuchochea maendeleo jamii na nchi kwa ujumla.