Na mwandishi wetu, Babati
EMMANUEL Philip Gekul, ambaye ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo amerejesha rasmi fomu yake baada ya kujaza na kukamilisha taratibu zote zinazohitajika.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Babati Vijijini, Gekul amesema ana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Babati Vijijini kwa uaminifu, uwazi na bidii kubwa.
“Nina moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi wa Babati Vijijini na kuchangia katika maendeleo yao. Nimeamua kurudi kuomba ridhaa yenu ili tuendelee pamoja na safari ya maendeleo,” amesema Gekul.
Fomu hiyo imepokelewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Vijijini, Aziza Isimbula.
Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM unatarajiwa kukamilika leo saa kumi na nusu jioni.