Afisa Ugavi Mwandamizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi (wa pili kulia) akipewa mkono wa pongezi na Msanii wa Sanaa ya Uchekeshaji, Bw. Mtanga Hamis, maarufu Mtanga,baada ya kupata elimu ya ugavi, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu, kulia ni Afisa Ugavi, wa Idara hiyo, Bi.Anne Swila na wa pili kushoto ni Msanii wa Sanaa ya Vichekesho, Bw. Dickson Malwaya, maarufu kama Bambo.
Afisa Ugavi Mwandamizi wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Bi. Vaileth Mwakajisi (kushoto) akimkabidhi kipeperushi, Bi. Maria Rafael, kinachohusu namna Wizara ya Fedha inavyosimamia mnyororo wa Ugavi, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Wizara ya Fedha, Bw. Fedrick Sanga, akitoa maelezo kwa Meneja wa Kanda ya Pwani wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Bi. Vick Mollel, kuhusu masuala ya Ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, akitoa elimu ya deni la Serikali na deni la Taifa, kwa mkazi wa Temeke Dar es Salaam, Bw. Bausi Matumbo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Boniface Kilindimo akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu kuhusu maandalizi ya bajeti ya Serikali.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Mifumo ya Kifedha na TEHAMA, Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga, akitoa elimu kwa mkazi wa Dar es Salaam, Bw. Jeremiah Sisya, namna ya kupakua GePG App, ili kurahisisha ufanyaji wa malipo ya Serikali, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Kumbukumbu kutoka Kitengo cha Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Stella Mtally, akijibu maswali kuhusu pensheni inayotolewa na Hazina kwa wananchi walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.
Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Mary Mihigo akitoa elimu kwa kazi wa Dar es Salaam, Bw. Sarah Njau, kuhusu akiba, mikopo na uwekezaji alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Fedha)
….