Mkuu wa Utumishi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti amehitimisha Mafunzo ya Askari wapya katika Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi iliyopo Kihangaiko , Msata Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, leo tarehe 28 Juni 2025.
Askari waliohitimu Mafunzo wamekula kiapo cha Utii mbele ya Mkuu huyo wa Utumishi Jeshini.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo, Meja Jenerali Gaguti amewataka Askari wapya kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo cha Utii walichokula na kuwa tayari muda wote kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Askari hao wametakiwa kuzitunza Afya zao kiakili na kimwili ili wakati wote wawe tayari kuilinda Mipaka ya Tanzania na kulitumikia Taifa.
Aidha Meja Jenerali Gaguti amewaasa Askari hao kuzingatia mambo manne kwa Mwanajeshi ambayo ni nidhamu nzuri, Utii, Uhodari na Uaminifu kwani Taifa linawaamini na kuwategemea.
Naye Mkuu wa Shule ya Mafunzi ya hawali ya Kijeshi Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala ameeleza kuwa Askari wapya wote wamefunzwa na kuhitimu kwa viwango vinavyokubalika