Na Ashrack Miraji Fullshangwe Media
Kada wa chama Cha mapinduzi mkoani Kilimanjaro, Iddy Mfinanga amechukua fomu ya kuwania Kuteuliwa kugombea udiwani katika kata ya makuyuni kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm.
Mfinanga alifika katika ofisi za ccm Kata ya Makuyuni majira ya saa mbili kamili za asubuhi akiambana na familia yake na kupokelewa na katibu wa kata wa chama cha mapinduzi ccm Mh Halidi Msangi na baada ya maelekezo mafupi alikabidhiwa form hiyo nakala tatu na kuondoka eneo la ofisi hizo za kata.
Aidha ndugu Iddy Mfinanga amekuwa kada wa kwanza kuchukua form katika kata hiyo ya makuyuni.