Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Hesabu, Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Mercelina Haule, akitoa elimu kuhusu masuala ya kiuhasibu na fedha katika Serikali kwa Msaidizi wa Mwasibu Mkuu wa Serikali, Usimamizi wa Fedha, Bw. Ayoub Banzi,(upande wa kushoto) alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Killo, akitoa elimu ya namna ya uondoshaji wa mali chakavu kwa Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma, ACP Eva M. Stesheni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Hazina Saccos, Dkt. Festo Mwaipaja, akieleza hatua za kujiunga na Saccos hiyo na faida zake kwa Bi. Fatuma Mshana, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Idara wa Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Daved Massawe, akitoa elimu kwa Bw. Ndarai Selenda kuhusu huduma zinazotolewa katika Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Taifa, Boniface Kilindimo, akitoa elimu kuhusu maandalizi ya bajeti ya Serikali na Usimamizi wake kwa Bi. Prisca Beresha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Afisa TEHAMA, Idara ya Mifumo ya Kifedha, Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga, akitoa elimu kwa Bw. Longiana Mjanaheri kuhusu maelekezo ya matumizi ya Aplikesheni ya Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki waliohudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha,Dodoma)
,………
Eva Ngowi na Chedaiwe Msuya, WF, Dodoma
Watumishi wa Umma wameaswa kuendelea kuzingatia miiko na maadili ya utumishi wa umma, sera za nchi, sheria, kanuni na miongozo iliyopo; ambayo inahitaji ukarimu, kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Maelekezo hayo yametolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) alipokuwa akihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa Mifumo ya Kidijiti kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa alisema ni vyema kuimarisha mikakati ya kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kutumia fursa za uwepo wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ili wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata huduma zinazotolewa na Serikali kwa haraka zaidi.
Wakati akizindua mfumo wa Kidijiti Mhe Majaliwa, alizitaka Taasisi zote za umma kutekeleza agizo la Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kuwa Taasisi zenye mifumo na zinazoendelea kubuni mifumo inasomana na zinaweza kubadilishana taarifa kupitia mfumo huo ili kuboresha huduma ndani ya Serikali.
“Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA hakikisheni kwamba mifumo iliyounganishwa inendelea na majukumu yake ya kubadilishana taarifa lakini pia kila anaeingia mjiridhishe kuwa ana uwezo wa kuwasiliana na yeyote alioko kwenye mfumo. Alisema Mhe. Majaliwa.
Vile vile Mhe. Majaliwa aliwaasa watumishi wa umma kote nchini kujisajili katika mfumo wa kidijitali wa e – wezesha, ambao unawezesha watumishi wa umma kuwekeza moja kwa moja kupitia makato ya mshahara au mapato mbalimbali ya biashara.
Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambayo yalianza tarehe 16 Juni, 2025 na kuhitimishwa leo tarehe 23 Juni, 2025 yameshirikisha Taasisi za Serikali 146, ikiwemo Wizara ya Fedha, pamoja na wafanyabiashara wa makundi mbalimbali