Baada ya uzinduzi wa Heineken Silver — kinywaji kipya chenye ladha laini na ubora usio na mpinzani — wakazi wa jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine wamekipokea kwa shangwe, wakisifu ubora wake na jinsi kilivyotengenezwa kwa viwango vya kimataifa.
Uzinduzi huo wa kipekee ulifanyika usiku wa kuamkia Juni 22, 2025 katika viunga vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya wageni 400 walipewa mwaliko kushiriki katika tukio hilo la aina yake.
Mastaa wakubwa wa Bongo, influencers maarufu, content creators wa kizazi kipya na mashabiki wa burudani kutoka kona zote za jiji.
Tofauti na matukio mengine, hakukuwa na sehemu ya VIP – kila mmoja alihudumiwa kama mgeni wa heshima, akipata huduma ya kifalme bila kujali jina au nafasi. Hali hiyo iliweka usawa wa kipekee na kuongeza mvuto wa hafla hiyo.
Wageni walijitokeza kwa mitindo ya kuvutia, wengi wakiwa wamevalia mavazi ya “Silver Futuristic” yaliyomeremeta kwa mwanga wa fedha, yakiangaza usiku mzima. Mwonekano huu wa kisasa uliibua ushindani mkali wa ubunifu wa mavazi, ambapo mshindi wa vazi bora alijinyakulia zawadi ya shilingi milioni 2 na sifa zote za usiku huo.
Kwa sasa, Heineken Silver inaendelea kusambaa kwa kasi, ikipokewa kwa mikono miwili na wapenzi wa vinywaji baridi kote nchini.