Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akisalimiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, kuhusu huduma zinazotolewa katika Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu (Mb) (kulia) akiagana na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Sepo Seni, baada ya kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bi. Stellah Mtally, akitoa elimu kuhusu Pensheni inayolipwa na Hazina kwa Wastaafu kwa Mkazi wa Dodoma Bw. Michael Mshana, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Wiki ya Utumishi wa Umma, viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Taifa, Boniface Kilindimo, akitoa elimu kuhusu maandalizi ya bajeti ya Serikali na Usimamizi wake kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Raphael Macha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma
Mtumishi wa Hazina Saccos, Bi. Leah Nkinda, akieleza hatua za kujiunga na Saccos hiyo na faida zake kwa Bi. Doroth Mayala, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. William Marwa, akitoa elimu ya namna ya uondoshaji wa mali chakavu kwa watumishi wa umma waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Grace Samwel, akitoa elimu ya uwekezaji kwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bw. Raphael Macha, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Maafisa kutoka Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
…………….