Aidha Naibu Waziri Katambi amewapongeza madereva hao kwa kuandaa kongamano hilo lenye dhamira ya kuipongeza serikali katika kazi kubwa iliyofanywa nchini.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Katambi amesema kuwa serikali inaendelea kusisitiza utoaji wa mikataba kwa madereva ili kuonyesha makubaliano kati ya mmiliki wa chombo na madereva.
“Ni muhimu sana kutoa mikataba kwa sababu inaonyesha haki ya wajibu kwa Mmiliki wa chombo na Dereva lakini usalama wa chombo ni kupitia mkataba”amesema Naibu Waziri Katambi
Awali akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando amesema kuwa watahakikisha wanaendeleza ushirikiano na madereva wote wanaofanya shughuli zao kwani Ubungo imekuwa ni lango la kwenda katika maeneo mbalimbali nchini
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Madereva wa masafa marefu na ya kati Tanzania Hassan Dede ametumia fursa hiyo kusema madereva wanakiu kubwa kuona mambo yanabadilika.
Naye Mrakibu wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania -Mussa Manyama amesema wao kama wasimamizi wa sheria wanawakumbusha madereva kuendelea kutii Sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali.
Amewataka kuondoka na kuendesha magari Kwa mwendo wa masi kwani imekuwa ni chanzo kikubwa cha ajali barabarani
Mr. Chuki Shaban ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Malori (TAMSTOA) amesema ni vyema wamiliki wote wa Malori kuingia kwenye Vyama ili kuweza kutambulika Kwa haraka.