Wanawake na Samia Takaribani 135 wanatarajia kunuifa na mpango wa masomo ya muda mfupi ,katika Chuo cha ufundi stadi Veta mkoani Mara, yanayofadhiliwa na na serikali ilikuwajengea ujuzi na kuinua uchumi wao kupitia fani mbalimbali ikiwemo umeme,udereva,upishi ,ususi na fani ambazo wataanza nazo.
Akizungumza mkuu wa chuo cha Veta Mara Martin Mollel alisema mafunzo hayo yatakuwa ya kuwawezesha washitiki hao kupata ujuzi wa ufundi, stadi za maisha pamoja na elimu ya ujasiriamali,kupitia ujuzi huu ,ambapo alisema walishiriki hao wataweza kujitegemea kiuchumi na kupunguza utegemezi kwa kundi hilo.
Katika mafunzo hayo jumla ya washiriki 485 watasajiliwa kati ya hao kina mama 135 wamefadhiliwa kwa asilimia 100 kupitia mpango wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan huku vijana wengine 350 wakifadhiliwa na TACAIDS kwa kushirikiana na Global Fund .
Mollel alisema washiriki hao wanatoka katika makundi ya vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 40 pamoja na kina mama walioko katika mazingira magumu na wasiokuwa na fursa katika mfumo rasimi wa elimu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya washiriki na wanufaika wamafunzo hayo samia na wanawake wamameshukuru Rais wa dkt Samia suluhu Hassan kwa sasa pindi watakapohitimu itawasaidia kuongeza thamani katika bidhaa zao pamoja na kufungua makampuni yatakayowasaidia kupata tenda maeneo mbalimbali ikiwemo serikalini.