Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima akifungua kongamano hilo jijini Arusha leo

Mkurugenzi wa mamlaka ya ununuzi wa umma Denis Simba alizungumza kwenye kongamano hilo jijini Arusha leo


………..
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Dkt Dorothy Gwajima ameziagiza halmashauri zote nchini kusaidia kuibua makundi maalumu ya kijamii katika maeneo yao ambayo yatajipatia fursa zilizotengwa na serikali kwa ajili yao pamoja na kuwataka wataalamu wanaojihusisha na ununuzi kuzigatia weledi wa taaluma zao na maadili.
Dkt Gwajima ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua kongamano la 9 la ununuzi wa umma la mwaka 2025(PPRA) kwa niaba ya Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba ambapo amesema kuwa wanapotumia fedha za umma kununua bidhaa, huduma au miradi wanapaswa kufahamu hitaji la maendeleo endelevu na ustawi kwa manufaa ya muda mrefu wa wananchi.
Dkt.Gwajima amesema kuwa ,Tanzania kama ambavyo nchi nyingi Duniani imetambua umuhimu wa matumizi ya TEHAMA katika ununuzi wa umma ambapo mifumo hii kwa kiasi kikubwa inaondoa changamoto ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele kwenye sekta mbalimbali.
“Tulikuwa tukipishana na magari kupeleka nyaraka, huku huyu hayupo, mara jaza mafuta yameisha, mzabuni anazusbiri tu,mara umekosea kujaza halafu makaratasi ambayo yangezalishwa yachanwe yachomwe na jambo ambalo lingesababisha athari ya mazingira,”amesema
Amesema kuwa Matumizi ya mifumo ya kieletroniki yakiendelea kuhamasishwa yana faida kubwa kwa serikali kama ambavyo tumeona NEST imeleta faida mbalimbali ikiwemo kupunguza athari za mazingira na kupungua kwa gharama za kuendesha zabuni za serikali ikiwa ni pamoja na kuondokana na matumizi ya karatasi, kuongezeka kasi ya ununuzi, kupungua makosa katika ununuzi, utuzaji bora wa kumbukumbu na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
“NEST imeongeza uwazi na uwajibikaji, imechangia kuleta thamani halisi ya fedha inayotumika katika ununuzi lakini pia mfumo huu unaleta faida nyingi na kuimarisha utawala bora pamoja na kuongeza wigo na ushindani na zaidi imesaidia mapambano dhidi ya rushwa, uzembe, udanganyifu na madhaifu katika ununuzi wa umma,”amesema .
Sambamba na hayo amezitaka taasisi za manunuzi kuhakikisha matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali katika ununuzi wa umma nchini pamoja na kutenga asilimia ya ununuzi wao kwa mwaka kwa ajili ya kampuni za wazawa na makundi maalum ili kuhakikisha zabuni zilizotengwa kwa wazawa zinatolewa kwa wazawa kama zilivyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mamlaka ya ununuzi wa umma Denis Simba amesema kuwa mfumo wa NEST ulianza kutumika rasmi Julai 1, 2023 ambapo hadi sasa mfumo una moduli 6 ambazo ni usajili wa watumiaji wa mfumo(e-registration) uchakataji wa zabuni kufanyika katika mfumo (e-tendernet), usimamizi wa mikataba(e-contract) ambayo imekamilika na inatarajiwa kuanza kutumika rasmi Julai, 2025.
“Katika moduli hii zipo moduli nyingine ndo tano ambazo ni uaandaaji wa mikataba, uanzishwaji wa mikataba, utekelezaji wa mikataba, malipo ya mikataba, usitishwaji wa mikataba na mabadiliko ya mikataba, unaona upana wa hii moduli ya e- contract na ndio maana ulituchukua muda kuweza kukamilisha,”amesema.
“Hapa tunazungumzia ujenzi wa shule darasa moja, ujenzi wa matĥundu ya vyoo, ununuzi wa bandari,ununuzi unaofanyika kwa wenzetu wa reli, ununuzi wa meli na ununuzi ambao unagusa maeneo mbalimbali,” ameongeza .
Aidha amesema kuwa hadi kufikia Juni 11,2025 wazabuni 38,163 waliidhinishwa na kusajiliwa ambapo kati ya hao 36,377 ni wazabuni wa ndani na 1,776 ni wazabuni kutoka nje ya nchi.
Ameongeza kuwa, jumla ya taasisi nunuzi 91,415 zikiwemo taasisi kuu za ngazi ya chini za serikali zamitaa zimesajiliwa kupitia mfumo wa NEST zikiwa na jumla ya watumiaji 131,202 ambao wamesajiliwa NEST.
Aidha ” kauli mbiu ya kongamano hilo ni “ununuzi wa umma wa kidigitali kwa maendeleo endelevu, ukuzaji wa kampuni za wazawa na makundi maalumu kwa ukuaji wa uchumi jumuishi.”amesema .