*๐ผ๐ฉ๐ค๐ ๐ค๐ฃ๐ฎ๐ค ๐ฉ๐๐๐๐ ๐ฎ๐ ๐ ๐ช๐ฉ๐๐ฃ๐๐๐ฃ๐๐ฏ๐๐๐ฃ๐ ๐ฉ๐ช๐๐ช๐ข๐ ๐ฏ๐ ๐ช๐ค๐ฃ๐๐ค ๐๐ก๐ ๐ ๐ช๐ฌ๐๐ ๐๐ฉ๐๐ ๐ฌ๐๐ฃ๐ฎ๐ ๐จ๐๐๐ ๐ฏ๐ ๐ ๐ช๐๐ค๐ข๐๐๐.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Oganaizesheni, Ndg. Issa Ussi Gavu, amesema ni marufuku kufanya vitendo vichafu na vya uonevu ikiwemo kuzushiana tuhuma kwa lengo la kuwawekea vikwazo wenye lengo la kugombea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ndg. Gavu amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitafumbia macho vitendo hivyo kwa kuwa kinataka wagombea watakaotokana na kura halali za ndani ya Chama ili kujihakikishia ushindi katika uchachaguzi huo.
Hayo ameyaeleza wakati alipokuwa na wanachama wa CCM Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam siku ya tarehe 14 Juni 2025 kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika hotuba yake, Ndg. Gavu ameendelea kuwahakikishia wana CCM wakiwemo wenye ni ya kugombea nafasi za ubunge na udiwani kuwa hakuna atakayekatwa kwa hila na uonevu.
Pia, alivitaka vikao vya uchujaji ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha vinatenda haki kuwapitisha wenye sifa na wenye kasoro mbalimbali waitwe, wasikilizwe, wapewe nafasi ya kujieleza na ikibidi kuadhibiwa waadhibiwe kwa haki.
โMsifanye mambo ya kihuni, yapo mambo ya kukata kihuni kwa chuki zenu ama rushwa, unaonekana unajaza fomu ukaambiwa wewe ni mwizi ukaitwa katika kamati ya maadili ukifika pale katika kamati ya maadili unaulizwa jina lako nani…unasomeka wewe una tuhuma, tuhuma zako hujasomewa huzijui unaambiwa tu hivyo bila uthibitisho, utaratibu huo mara hii ukome.โ
Vilevile, Ndg. Gavu alitumia mkutano kuwatumia salamu kuwa CCM imedhamiria kutafuta viongozi wenye sifa, wasio na makandokando.
โTuna wanachama zaidi ya milioni 13, nafasi za ubunge zipo nafasi 282, nafasi za udiwani zipo 4,030 kwenye kata na viti maalumu, hii maana yake nafasi moja ya ubunge ina watu zaidi ya 42,000, hatuwezi kukosa mtu mwenye sifa ndani ya watu 42,000 kwenda kutuwakilisha.โ