Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametembelea familia na kuweka Shada la Maua katika kaburi la aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Hayati Mzee Cleopa David Msuya katika Kijiji cha Chomvu Usangi Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro.
Katika salamu zake za pole kwa familia, Waziri Mkenda amesema kuwa Hayati Msuya alikuwa kiongozi mahiri na mzalendo kwa Taifa.