Wataalamu wa TEHAMA katika Sekta ya Maji kuongeza nguvu katika kuhakikisha mifumo ya kidigiti inasomana kuendana na teknolojia inavyokua.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema hayo Mtumba, jijini Dodoma na kuongeza kuwa hatua hiyo itarahisisha kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma ya maji kwa haraka.
Akiongea na wataalamu hao amewataka kutafuta namna bora itakayowezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu masuala ya huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kupitia mifumo.
“Hakuna sababu ya kuanza kuzitafuta taarifa za hali ya huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwenye makaratasi au kwa watu,haya yanaweza kufanyika kupitia mifumo iliyo jitosheleza.” Mhandisi Mwajuma amesema.
Pamoja na hilo, awamewapongeza wataalamu wote kwa jitihada wanazo zifanya katika kuhakikisha lengo na mkakati wa Wizara ya Maji yanafanikiwa kupitia TEHAMA.