Jumla ya mabondia 144 kwa mchanganuo wa wanaume 136 na wanawake 8 wamefuzu vigezo kuendelea kushiriki mashindano ya wazi ya ubingwa wa Taifa 2025 katika ukumbi wa Manyara Park uliopo Tandale jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo yalianza jana tarehe 2/6/2025 kwa zoezi la usajili kwa washiriki wote, zoezi lililoendelea hadi leo saa 6.00 Mchana.
Kesho kuanzia 8.00 Mchana tutaanza rasmi mashindano haya rasmi, kwa hatua ya mtoano.
Ratiba ya mabondia wote watakaocheza kesho imeambatanishwa katika taarifa hii na wote wanatakiwa kufika katika ukumbi wa mashindano kesho kuanzia saa 2.00-4.00 Asubuhi kwa ajili ya zoezi la kupima afya na uzito.Saa 8.00 kamili pambano la kwanza linaanza. Jumla ya timu 15 kutoka mikoa mbalimbali zimeshiriki mashindano.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu- BFT.