Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Mheshimiwa Ichiro Aisawa, Mwenyekiti wa Chama cha Urafiki wa Wabunge wa Japan na Afrika (Africa Union Parliamentarians Friendship) kwenye Ofisi za Bunge la Japan, Mei 29, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza na Mheshimiwa Ichiro Aisawa, Mwenyekiti Chama cha Urafiki wa Wabunge wa Japan na Afrika (Africa Union Parliamentarians Friendship) kwenye Ofisi za Bunge la Japan, Mei 29, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Ichiro Aisawa, Mwenyekiti Chama cha Urafiki wa Wabunge wa Japan na Afrika (Africa Union Parliamentarians Friendship) (Wa pili kulia) na ujumbe wake, kwenye Ofisi za Bunge la Japan, Mei 29, 2025. Kushoto ni Naibu Waziri , Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
.…………..
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Mei 29, 2025 alikutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Japan cha Urafiki na Afrika (Africa Union Parliamentarians Friendship) Mheshimiwa Ichiro Aisawa, kwenye Ofisi za Bunge la Japan.
Katika mazungumzo yao walijadili kuhusu kuendeleza urafiki kati ya Bunge la Tanzania na Bunge la Japan.
Pia, walijadili kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Japan, pamoja na kumkaribisha kutembelea Tanzania ili kujionea vivutio mbalimbali ya utalii.