MAPUTO 28 Mei, 2025:
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha nchini Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Col. (Rtd) Donat Ndamage, Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Msumbiji.
Mkutano huo ni sehemu ya zoezi la kujitambulisha rasmi katika Jumuiya ya Mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini Msumbiji. Katika mazungumzo yao pia walisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa ukaribu kwa maslahi ya Serikali na Wananchi wa nchi hizi mbili.