Aliyekuwa Mkurugenzi wa Africa Media ambaye kwa sasa ni Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Bw. Shaaban Kissu akimkabidhi ofisi Kaimu Mkurugenzi mpya wa Africa Media Group Bw Dennis Msaky ambaye ameteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo, Kabla ya Uteuzi huo Dennis Msaky Alikuwa Katibu Msaidizi-Habari ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt.John Emmanuel Nchimbi
Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi imefanyika katika Ofisi za AMGL, kampuni inayomiliki vyombo vya habari vya Channelten, Magic FM na Channelten Plus.