Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia ziara ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah tarehe 20 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Bi. Salama Salehe Ghulum (Mama Salehe) na Bi. Rafran Ismail Khan ambao walikuwa majirani zake wakati akiishi Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam katika miaka ya 1980s. Mhe. Rais Dkt. Nandi-Ndaitwah alikutana na jirani yake huyo wa siku nyingi katika hafla ya chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mhe. Mama Gertrude Mongella kwenye hafla ya chakula cha jioni alichoandaliwa na mweji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amkaribisha Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah, Ikulu Jijini Dar es Salaam.