Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa na nzuri aliyoifanya ya kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika halmshaur hiyo.
Ambapo wamechangia kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle kuchukua fomu ya kugombea ubunge.
Akizungumza leo katika kikao cha robo ya tatu cha Baraza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mhe. Eliya Kgoma,amesema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa ya maendeleo wilayani humo.
Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji wa halmsahuri hiyo, Dkt.Semistatus H. Mashimba akizungumza kwa niaba ya watendaji wa Halmashauri,amesema kuwa wanaungana na Baraza hilo katika kumpongeza Rais Samia kutokana na fedha nyingi alizoleta kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambazo zimewanufaisha wananchi.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kasulu,Jennifer Chinguile,amepokea mchango huo kwa niaba ya chama na kuahidi kuuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM,Balozi Emmanuel Nchimbi kabla ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwezi huu.
Kwa upande wake,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Simon Nzibuje ametoa shukrani kwa mchango huo na kuhaidi kuufikisha kwa mhusika.
Akitoa salamu za serkali, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kuwa na taadhari na kuhakikisha wanatunza chakula kutokana na hali isiyoridhisha ya usalama wa chakula kwa sasa.