Wahifadhi tfs sao hill wakagua ukarabati wa miondombinu ya
barabaratarafa ya nne ya shamba mgololo akiwa katika eneo la ukaguzi wa barabara
Wahifadhi tfs sao hill wakagua ukarabati wa miondombinu ya barabaratarafa ya nne ya shamba mgololo akiwa katika eneo la ukaguzi wa barabara
Na Fredy Mgunda,Mufindi.
Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa mawasiliano ya barabara zilizopo ndani ya msitu yanaendelea kuwepo ili kuhakikisha shughuli za shamba na zile za watumiaji wa barabara hizo ambao ni wavunaji wa miti wanaosafirisha malighafi za miti wanapita katika barabara hizo bila vikwazo vyovyote.
TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza ili kuhakikisha wadau wanaovuna malighafi katika Shamba wanafanya shughuli hiyo kwa wakati na hivyo kupekelekea uvunaji na usafirisha wa malighafi unafanyika bila vikwazo, na kupelekea wadau hao kufanya shughuli zao kwa wakati za kujipatia kipato kwa kuvuna malighafi ya miti na pia serikali kukusanya mapato yake kwa wakati uliopangwa.
Shughuli mbalimbali zinaendele hapa TFS – Shamba la miti Sao Hii katika Tarafa zote nne (4) za shamba ikiwa ni pamoja na maandalizi ya bustani ya miche ya miti kwaajili ya msimu ujao wa upandaji na uvunaji wa malighafi ya miti katika kipindi hiki ambacho mvua katika baadhi ya maeneo zinaendelea kunyesha.