Kyerwa , Kagera
Wakulima wa zao la kahawa katika halmashauri ya kyerwa mkoani kagera wameomna kiwepo kwa mikopo itakayowasaidia katika kilimo cha kahawa kama yalivyo mazao mengine katika jaminnn.
Hayo yamezengumzwa katika mkutano wa adhara uliowakutanisha wananchi na timu ya msaada wa kisheria uliofanyika katika soko la kijiji .Nyamiaga kata bugomora wameiomba serikali kupitia katika kampeini ya msaada wa kisheri ya mama Samia na kusema kuwa serikali ingewatazama kwa jicho la tatu kwa kuwapatia pembejeo licha kuongezeka kwa thamani ya zao bado wanakutana na changamoto nyingi hasa ukifika msimu wa kuandaa mashamba ya kahawa kwani hawana pembenjeo za kisasa zitakazowawezesha kupata mavuno mengi zaidi.
Joseph Aloiz ni mmojawapo ya wakulima wa zao hilo amesema licha kuwepo kwa uhitaji wa pembejeo hizo bado jamii inapitia changamoto nyingi juu ya kahawa kwani zao hilo pia linasababisha migogoro ya ndoa, mirathi na kupelekea kufanya makosa ya kijinai bila wananchi kutambua.
” Kwanza nianze kushukuru Rais wetu Mama Samia kwani wananchi wengi asa wanaume walikuwa awajui kama kahawa nayo ni mali ya ndoa kwani kupitia kahawa wanandoa wanagombana na familia zinaharibika kwa migogoro hiyo hasa upande wa ardhi tulikuwa atujui ni nani ana jukumu la kuvuna kahawa na kuuza, Kupitia kampeini ya msaada wa kisheria ya mama samia naweza kusema nimeelewa zaidi kwani hata wananchi wenzangu watakuwa wamefunuliwa akili juu ya mali za wanandoa hata mashamba ya kahawa nayo ni mali ya wanandoa na katika uuzaji wa chochote niwasihihi wananchi wenzangu hakikisha unamshirikisha na mwenza wako” Bw. Joseph Aloiz.
Pia ameongeza kuwa elimu hii isi mwisho bali yawepo madawati ambayo yanendelwa kuweka usuruhushi katika jamii yao kwan hii inaweza kuchangia kuwa chachu ya maendeleo katika jamii na mkoa kwa ujumla.
Nae bi kasilida Chimagi ambae ni mratibu wa kampeini hiyo ya msaada wa kisheri ya mama Samia katika halmashauri ya kyerwa amewataka wananchi kutengeneza jamii yenye haki,usawa na maendeleo maana ndio hazima kuu ya kampeini hiyo ni kuhakikisha wanalinda ndoa zao na kuzitunza kwa amani bila kuwepo migogoro ya aina yoyote katika jamii.
Amewataka kuhakikisha elimu hiyo ya msaada wa kisheria inakuwa chachu ya maendeleo na kuelewa kuwa sheria inamtaka kila mwanandoa kushiriki kikamilifu katika mali zilizopatikana wakati wakiwa wote katika uendelezaji wa familia.