Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 15 kwa kuwa mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Shule za Afrika (CAF African Schools Football Championship) kwa mara ya pili mfululizo.
Rais Samia ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram akisema Ninajivunia ushindi wenu kwani ni fahari kwa Taifa letu na chachu ya kuendelea kukua kwa sekta ya michezo nchini.
Pia, ameipongeza na kuitakia kila la kheri Timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal kwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Women’s Futsal Cup of Nations 2025). Watanzania tunawaunga mkono, endeleeni kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.