Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidori Mpango amewasili katika Viwanja vya Santa Pedro, Vatican tayari kwa kushiriki maadhimisho ya Misa ya Mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francisko.
Mhe. Dkt. Mpango katika maadhimisho ya Misaa hiyo ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameungana na Marais na Makamu Rais 123 kutoka sehemu mbalimbali Duniani wanaoshiriki katika mazishi hayo ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani.