OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEM Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya afya kwa kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa, vifaa tiba na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya kwa ajili ya hospitali za Wilaya nchini ikiwemo Hospitali ya Mabogini.
Mhe. Katimba ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Zuena Athuman Bushiri aliyeuliza.
“Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la wagonjwa, vifaa tiba na wataalam katika Hospitali ya Wilaya ya Mabogini, Moshi Vijijini?”
“Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22 ilinunua magari 594 (ambulance 382 na, usimamizi 212) ya kubebea wagonjwa na usimamizi wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imepokea magari 2 ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Kituo cha afya cha Umbwe na Himo.” Amesisitiza
Amesema Hospitali ya Wilaya ya Mabogini katika mwaka wa fedha 2024/25 imepelekewa shilingi milioni 165 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Aidha, vifaa tiba vimeshanunuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mabogini.
Hospitali ya Mabogini inajumla ya watumishi saba (7) wanaotoa huduma katika hospitali hiyo kwa sasa.