Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Nyasa Bw. Jacob Benworth Kunani tarehe 25.04.2025 amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika katika Ofisi za Umoja wa Vijana UV-CCM Wilaya ya Nyasa.
Akikabidhi Kadi yaCHADEMA Na kupokea Kadi ya CCM Bw. Kunani amesema anayofuraha kubwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Viongozi wa UV-CCM Wilaya ya Nyasa na kusema kuwa amepata amani ya roho, kwa kuwa Chama cha Mapinduzi ni chama imara kinachoendeshwa kwa misingi ya amani na Utulivu NA Kiko kwa ajili ya kujenga Taifa na kuleta Maendeleo ndani na nje ya Tanzania.
Ameongeza kuwa amejikuta ametoka kifungoni na sasa yuko huru, hata hivyo ameahidi kuwa atashirikiana vema na wanachama wa CCM.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ni Komred Clavian Matembo mwenyekiti wa Umoja waVijana UV-CCM Wilaya ya Nyasa amempokea na kumkaribisha CCM na kumtaka awe mwanachama mwaminifu na kumsajili katika Mfumo wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano ili mawze kupata kadi ya CCM pamoja na kumpa Tisheti ya Chama Cha Mapinduzi.