Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya ustawi wa jamii ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Sabiha Filfil Thani na Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakiwa katika ziara ya kukagua Kiwanja cha Mao-zedong na Tume ya Utangazaji Zanzibar.
……….
Zanzibar.
Kamati ya kudumu ya ustawi wa jamii ya Baraza la Wawakilishi, imeitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuiwezesha Tume ya Utangazaji Zanzibar kupata vifaa vya kiasasa ili iweze kukabiliana na wakati uliopo wa sayansi na teknolojia.
Mwenyekiti wa Katami hiyo Mhe. Sabiha Filfil Thani amesema hayo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, kwa kipindi Cha Robo mwaka, kuanzia Januari hadi machi 2025 huko Muembemadema Wilaya ya Mjini.
Amesema, Tume hiyo inakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo Wataalamu, Vifaa vya kisasa na Ofisi hivyo iwapo iwapo itawezeshwa itaweza kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Aidha ameiagiza Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo kusimamia masharti ya Tume ya Utangazaji Zanzibar ili kulinda Mila, Silka na Utamaduni wa Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita, amesema Tume ya Utanagazaji Zanzibar, imeweza kukaguwa vituo 38 vya matangazo na kuwahamasisha kufuata masharti na Taratibu za Tume ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza ikiwemo kufungiwa.
Amesema Tume, imefanikiwa kuongeza usikivu wa vituo vya Redio za Fm baina ya Tanzania bara na Zanzibar ambapo imeviwezesha vituo vya Zanzibar kutoa habari Jijini Dar-es-salaam.
Mkurugenzi idara ya Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Rashid Hamdu Makeme ameipongeza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango kwa mwaka huu kuwapatia jumla ya Gari 9 ambapo zimepunguza tatizo la usafiri.
Nae, Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Hiji Dadi Shajak amesema Tume hiyo, imeweza kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada za leseni ambapo imefanikiwa kukusanya Zaidi ya asilimia 128.
Amebainisha kuwa kuwa, mafanikio hayo yametokana na usimamizi na ufuatiliaji nzuri wa Madeni katika vituo mbali mbali vya Utangazaji.