Na Sabiha Khamis Maelezo 25/04/2025.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe Shariff Ali Shariff amezitaka taasisi binafsi vyama vya wafanyakazi na mashirika ya kimataifa kushirikiana katika kuandaa mazingira salama katika kazi na yenye kuzingatia haki za kibinaadamu ili kuweza kulinda afya na usalama wa wafanyakazi.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini ambapo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 28 April, katika ukumbi wa Wizara hiyo Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B amesema siku hiyo imewekwa rasmi na shirika la wafanya kazi Dunia (ILO) ambapo huadhimishab siku hiyo kwa lengo la kuhamasisha ukingaji wa ajali, maradhi na vifo vinavyotokana na sehemu ya kazi.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua kuwa teknolojia ya kisasa ni injini ya maendeleo, ila pamoja na furza zake pia inaweza kuleta changamoto hivyo ni wajibu kukabiliana nazo kwa weledi na mikakati ya kisera, miongoni mwa teknolojia hizo ni pamoja na automatic ya kazi, vifaa mahiri na mfumo wa utekelezaji wa moja kwa moja.
Aidha Mhe. Shariff ameeleza Wizara imejipanga kuzingatia mambo muhimu katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuboresha Sera sheria na miongozo ili ziendane na maendeleo ya teknolojia, kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika teknolojia salama katika mazingira ya kazi, kutoa mafunzo ya kidigitali kwa wakaguzi na wataalamu ili kuendana na wakati na kuhakikisha ujumuishwaji wa makundi yote wanawake, vijana, walemavu na wafanyakazi wasiokuwa katika sekta rasmi.
Hata hivyo amewataka wafanyakazi kufuata malekezo ya usalama na kutumia vifaa vya kujikinga pamoja na kuripoti kazini kwa waajiri na viongozi, kutoa vifaa vya kinga pamoja na kuunda sera, kutoa mafunzo mara kwa mara na kuhakikisha mazingira bora ya kazi sambamba na kuwasisitiza waajiri kutoa vifaa kwa wafanyakazi na kuweka sera madhubuti za usalama na kuhakikisha mazingira bora ya kazi.
Madhimsho ya siku ya usalama na afya kazini duniani kwa mwaka huu yameambatana na kauli mbiu “Teknolojia mpya na mustakbali wa usalama na afya kazini”.