Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana amekipokea kikosi cha timu ya Simba mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini humo kabla ya kuanza safari ya kwenda Durban ambako Simba itacheza mchezo wa raundi ya pili ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Timu ya Stellenbosch linaloandaliwa na Shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Amani Complex visiwani Zanzibar Simba iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Stellenbosch ya Afrika Kusini Balozi Bwana amepata nafasi ya kuzungumza na viongozi, benchi la ufundi na wachezaji.