……
MWENYEKITI wa Bodi ya Benki ya Ushirika (COOP Bank)Prof.Gervas Machimu amesema maandalizi ya uzinduzi wa Benki hiyo yanaendelea vizuri na hadi sasa kufikia asilimia 70.
Benki hiyo inatarajia kuzinduliwa rasmi Aprili 28,mwaka huu na Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na wanaushirika kutoka mikoa mbalimbali.
Akizungumza katika mahojiano maalum na waandishi wa habari amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa benki hiyo.
Amesema tayari maandalizi yamefanyika kwa asilimia kubwa huku akisisitiza wanaushirika kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa benki hiyo.
Prof.Gervas amesema benki ya ushirika ya taifa ilianza Oktoba mwaka huu na nimuunganiko wa benki mbili za ushirika ya Tandahimba na Kilimanjaro.
“Benki hizi mbili zilikuwa zikifanya biashara maeneo ya kimkoa hivyo tukaamua kuziunganisha na kupata benki moja ambayo itafanya kazi nchi nzima.
“Asilimia 51 ya benki inamilikiwa na vyama vya ushirika huku mtu mmoja mmoja nao wananafasi ya kushiriki ambapo wanaasilimia 49 hii inafanya ushiriki kuwa mkubwa zaidi,”amesema.