Klabu ya Leicester City imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu ya England (Premier League) hadi Championship baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Liverpool.
Leicester City walikuwa nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Premier League walipomfuta kazi kocha Steve Cooper uamuzi ambao sasa unaonekana kama kosa kubwa.
Walimleta Ruud van Nistelrooy kwa matumaini ya kuokoa jahazi, lakini hali ilienda kuwa mbaya zaidi.
Van Nistelrooy ameshinda mechi mbili pekee, na hatimaye ameishusha daraja huku zikiwa zimebaki mechi tano kumaliza msimu.
Uongozi wa Leicester sasa unakosolewa vikali kwa kumfuta kazi kocha Cooper ambaye alikuwa bado na matumaini.
Kutoka kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England mwaka 2016, hadi kushuka daraja kwa maamuzi mabovu.