Balozi wa Tanzania nchini Sweden Balozi Mobhare Matinyi akisaini kitabu cha maombolezo katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania miaka mingi Marehemu Hashim Lundenga ambaye alifariki Aprili 19, 2025 katika hospitali ya Kitemgule Tegeta jijini Dar es Salaam.
Mwili wa Hashim Lundenga umeagwa leo nyumbani kwake Mnara wa Voda Bunju na kusafirishwa kwao Ifakara mkoani Morogoro kwa Mazishi ambayo yatafanyika kesho Aprili 22, 2025, Mungu aiweke Mahali Pema Peponi Amen.
Picha zikionesha Gari lililobeba mwili wa Marehemu Hashim Lundega iliwasilisha nyumbani kwake Bunju Mnara wa Voda huku waombolezaji wakishusha mwili kwenye gari na kuingiza katika nyumba yake kwa mara ya mwisho.
Kutoka kuli ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden Balozi Mobhare Matinyi, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Bw. Ephraim Mafuru na Bw. David Minja wakiungana na waombolezajibalimbali katika msiba huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani na Maridhiano Sheikh Alhad Mussa Salum akitoa mawaidha katika msiba huo.
Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mobhare Matinyi akisalimiana na Mkurugenzi wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku wakati alipofika kuaga mwili wa marehemu Hashim Lundenga nyumbani kwake Bunju Mnara wa Vodacom.
Bosco Majaliwa aliyekuwa Mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania akiwa na waombolzeaji waliomuwakilisha Balozi Hoyce Temu. Naibu Mwakilishi wa Kudumu UN Geneva- Uswisi na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1999 kulia ni Aneth Andrew Temu na katikati ni Sara Andrew Temu.