Mbunge wa viti Maaalum Mkoa wa Mara Ghati Chomete amesema kamwe hatakuwa Bubu katika kudai utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwania ya wanamara kutokana na dhamamana kubwa waliyoiomba kwa wananchi.
Ghati ametoa kauli hiyo katika kata ya Bwiregi Wilayani Butiama Mkoani Mara ,wakati wa usomaji wa utekelezaji wa ilan ya Chama cha Mapinduzi ambapo amesema kata ya Bwiregi imepokea zaidi ya shilingi Bilioni 2.215,283,736.39 katika kipindi cha mwaka 2020-2025.
Alisema kamwe hatakuwa Bubu kuiomba serikali kutatua changamoto kzinazoukabili Mkoa wa mara katika Sekta ya Maji,Elimu,Afya pamoja na Barabara ambapo alisema viongozi wanawajibu wakuhakikisha changamoto zinazowakabili Wananchi zinafikishwa panapotakiwa.
” Ametuletea fedha nyingi kwenye Mkoa wetu wa mara katika hili tunalojukumu la Kumuunga mkono hasa Sisi wanachama wachama cha Mapinduzi tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 kwenda kufanya kweli” Alisema Ghati Chomete Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara.
Chomete amewataka akina mama na watanzania kutembea kifua Mbele kutokana na imani kubwa aliyoitengeneza ambayo kamwe haikutarajiwa na wengi alipoingia madarakani.
Kwa upande wake Diwani wakata ya Bwiregi Nyageti amesema Tayari wamepokea fedha kwaajili ya ujenzi wa Madarasa,miradi ya maji utekelezaji wa miundombinu ya Barabara.