Simba Sc imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1 -0 dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa leo Aprili 20, 2025 Visiwani Zanzibar.
Bao la Simba limefungwa na mchezaji Jean Charles Ahoua dakika ya 45 + 2 kipindi cha kwanza, goli ambalo limeduma kwa dakika 90 katika mchezo huo.
Baada ya mchezo huo wa awamu ya kwanza, Simba Sc watalazimika kusafiriki kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kucheza mchezo wa awamu ya pili utakaochezwa Aprili 27, 2025 na mshindi wa jumla atatinga hatua ya fainali katika kombe hilo.