Na Prisca Libaga, Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini tarehe 16.04.2025 imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Nyumba Mbili za Upataji Nafuu zinazokaliwa na Wanaume na Wanawake zilizopo Olmotonyi na Moshono jijini Arusha.
Lengo la kutoa msaada huo kwa waraibu hao ni kuonesha kuwathamini, kuwajali, kuwapenda na kuwatia moyo waraibu wanaoendelea kupata nafuu katika nyumba hizo pamoja na kuwaonesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja nao katika mchakato wa kupona uraibu wa dawa za kulevya.
Aidha, Ofisi za DCEA na MAADILI Kanda ya Kaskazini zimetoa wito kwa wananchi kuendelea kukuza maadili yaliyokuwa mema katika jamii sababu maadili mabaya ndo sababu ya maovu yote katika jamii ikiwepo kujihusisha na matumizi au biashara haramu ya dawa za kulevya.



