Kufuatia kifo cha Ajali cha aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo -Hanga Mkuu wa Mkoa wa mara amemwagiza kamanda wa polis Mkoa wa mara kuchukua hatua Kali kwa wanaovunja Sheria za Usalama barabaran,huku akiitaka kila Mtumiaji wa Barabara kufata Sheria.
Kanali Mtambi ametoa kauli hiyo Wakati wa mazishi yaliyofanyika katika eneo la Migungani wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo amesema kamwe hatarajii kuona matukio ya Ajali zinazosabishwa na uzembe wakutokufuta Sheria za Usalama barabarani.
“Wanasema kila kila linapokuja swala lakifo nimpango wa Mungu Sawa hatukatai lakini kuna matukio yanasabajishwa na uzembe nitake kamanda wa polis Mkoa huu wa mara kufanya Oparesheni Kali kwa wanaovunja Sheria na kuwachukulia hatua Kali za kisheria”Alisema kanali Evans Mtambi Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo -Hanga alifariki Dunia Usiku wakumkia April 13 katika eneo la Nyatwali Wilayani Bunda Mkoani Mara baada ya gari lake kumkwepa mwendesha Baiskel kisha kugongangana uso kwa uso na Lori nakupoteza maisha yeye na Dereva wake.