VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
Jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo imetumia wiki ya maadhimisho ya wazazi kwa kufanya ziara ya kwenda kutoa msaada wa matofali elfu moja na mifuko ya saruji kwa ajili ya kusapoti mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kondo iliyopo katika kata ya Zinga pamoja na mifuko ya saruji kwa lengo la kuweza kuwasogezea huduma wananchi kuondokana na adha na kero ya kutembea umbari mrefu.
Pia Jumuiya hiyo wa wazazi imeweza kutumia wiki ya maadhimisho hayo kwenda kuzindua mradi wa duka la jumla na rejareja ambalo litakuwa likiuza bidhaa mbali mbali ikiwemo nguzo za chama,pamoja na vifaa vingine ikiwemo pamoja na kwenda kufungua shina la wakereketwa la kibulu la wafugaji.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maaadhimisho hayo ameweza kuambatana na viongozi mbali mbali wa jumuiya mbali mbali ikiwemo wenyeji ambao ni jumuiya ya wazazi na kufanya ziara kwa ajili ya kutembelea miradi hiyo ya kitega uchumi.
Mwenyekiti Mlawa ameipongeza kwa dhati jumuiya ya wazazi kata ya Zinga kwa kuweza kutekeleza ilani kwa vitendo ikiwemo kuweka mikakati madhubuti ya kuweza kuanzisha vitega uchumi vyao ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikni na kuondokana na kuwa tegemezi.
“Kwa kweli mimi nimefarijika sana kuungana na jumuiya ya wazazi katika kuadhimisha wiki yao na mimi nimeungana nao na kwa kweli nawapongeza sana kwa kuweza kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kwa ajili ya vitega uchumi ikiwemo kufungua duka kubwa la nguo na vifaa mbali mbali vya ccm kwa hiyo nina imani na kata nyingine zitaweza kuiga mfano huo kama walivyofanya kata ya Zinga.
Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa katika Wilaya ya Bagamoyo wameweza kujipanga kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo wamemejipanga vya kutosha kumsapoti na kumpa kura nyingi za kishindo cha zaidi ya asilimia 96 Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kadhalika Mwenyekiti huyo katika kuhakikisha kwamba anaiboresha jumuiya hiyo na kuiimarisha ameamua kuchangia mabati 72 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa nyumba ya katibu ya jumuiya ya wazazi ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kwa mtendaji huyo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ambapo pia ameahidi kuwasaidia kuwapa sapoti ya kuwaongezea mtaji wa bidhaa katika duka hilo.
Kwa upande wake Katibu wa umojawa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Bagamoyo Halima Dosa amebainisha kwamba lengo lao kubwa la jumuiya hiyo ni kuhakikisha kwamba kila kata inakuwa na vitega uchumi mbali mbali ili kuweza kuondokana na kuwa tegemezi na kuondokana wimbi la umasikini.
Alisema kwamba ameridhishwa na viongozi wa jumuiya ya wazazzi Kata ya Zinga kwa kuamua kusaidia jamiii ikiwemo kutoa matofali elfu moja kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ikiwa pamoja na kuzindua mradi mwingine wa duka ambalo litakuwa linauza bidhaa mbali mbali pamoja na nguo za chama.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Kata ya Zinga Hassan Kashingo amebaisha kwamba katika Kata ya Zinga wamejipanga na kuweka mikakati madhubuti ikiwemo kuwa ni mradi mbali mbali ya kitega uchumi amabyo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kukuza uchumi kwa jumuiya ya wazazi.
Maadhimisho ya wiki ya wiki ya jumuiya ya wazazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo yamefanyika katika eneo la viwanja vya Mnada wa mbuzi,na ng’ombe lililopoKata ya Zinga na kuhudhuria na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumjiya zake ikiwemo viongozi wa serikali pamoja na wananchi kutoka kata zote 11.