Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akipokea ripoti ya kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika nchini Comoro mwaka 2024 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kupitia na kupokea ripoti hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisiya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wataalamu wa afya walioshiriki kambi maalumu ya matibabu iliyofanyika nchini Comoro mwaka 2024 wakati wa kupokea ripoti ya kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo ilifanywa na wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).