Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya Habari , Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla hiyo jijini Arusha .

Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda akizungumza katika hafla hiyo jijini Arusha .



………..
Happy Lazaro, Arusha .
Waziri wa mawasiliano na teknolojia ya Habari , Jerry Silaa amesema kuwa, bado kuna changamoto kubwa ya pengo la kijinsia katika.sekta ya Tehama ambapo tafiti mbalimbali.zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake na wasichana wanaochagua taaluma ya Tehama bado ni ndogo ikilinganishwa na wavulana.
Ameyasema hayo jijini Arusha katika hafla ya kufunga mafunzo ya Tehama kwa zaidi ya wasichana 200 kutoka shule za sekondari za umma katika mikoa 31 bara na visiwani .
Silaa amesema kuwa ,kutokuwa na usawa huu kunapunguza nguvu kazi ya baadaye ya Taifa na dunia kwa ujumla .
“Hatuwezi kufikia malengo ya kidigitali ya kweli bila kushirikisha kimalifu wasichana na wanawake kwa kuwapatia wasichana wetu maarifa ya msingi ya Tehama na kuwajengea msingi wa kujiamini kufikiri kwa ubunifu,na kuwa sehemu ya kizazi cha ubunifu wa teknolojia .”amesema Silaa.
Amesema kuwa, wasichana hao kutoka mikoa 31 wameshiriki katika mafunzo haya na wanafunzi 48 walifanya mafunzo katika kituo cha DIT kampasi ya Mwanza ,kituo cha Donbosco Arusha kikiwa na wanafunzi 49,kituo cha Udom wanafunzi 40 ,MUST Mbeya wanafunzi 40,DIT Dar es salaam wanafunzi 39,na kituo cha Tehama Dimbani Zanzibar kikiwa na wanafunzi 40 ambao wamepata mafunzo kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa waote (UCSAF ).
Amefafanua kuwa, dunia ya sasa imefunguka kwa kasi na kila fursa muhimu ya kimaendeleo inahusisha matumizi ya Tehama ,hivyo mafunzo haya waliyoyapata ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mafanikio na ni msingi wa kuwajengea mwelekeo sahihi na ujasiri wa kujiamini kwa nyinyi wasichana kwani wana uwezo mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika.mabadiliko ya teknolojia yanayoikumba nchi na dunia kwa ujumla.
Amesema kuwa, ni matumaini makubwa kuwa wataendelea kutumia ujuzi huu wa kujifunza kwa vitendo na kuwa mabalozi wa Tehema katika shule zenu na jamii kwa ujumla.
Aidha amewataka pia kuhamasisha wasichana wengine kuondoa hofu kuvuka vizingiti vya kijamii na kuingia kwa hali katika fani ya Tehama .
“Tunatarajia mtaendelea na juhudi za kujifunza zaidi kuchagua mafunzo ya Tehama katika.elimu za sekondari ,vyuo na hatimaye kuwa sehemu ya wataalamu katika sekta muhimu.ya maendeleo ya Taifa.”amesema .
“Dunia inahitaji mawazo yenu ,ubunifu wenu, na nguvu zetu katika kutengeneza suluhishi la kidigitali kwa changamoto za kijamii na kiuchumi, na kumbukeni Tehema sio kwanajili ya wavulana tu bali ni kwa ajili.yenu nyote hivyo mliopewa fursa hii ni wajibu wenu kuitimia kwa lengo la kujenga mustakabali bora wa Taifa letu .”amesema .
Naye Mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda amesema kuwa,mfuko wa mawasiliano kwa wote mbali na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kama ujenzi wa mradi wa minara 758 katika kata 713 inatekeleza miradi mingine mbalimbali mojawapo ukiwemo huu wa Girls in ICT hii ni moja ya utekelezaji wa mkakati wa uchumi wa kidigitali ambao ulizinduliwa mwezi julai 2024 na Mhe.Rais Samia suluhu Hassan .
Amesema kuwa, mfuko huo umeandaa mafunzo kwa wanafunzi wa kike ili kuwajengea ujuzi na uwezo pamoja na kuhamasisha wasome mafunzo ya Tehama ambapo mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya msichana na Tehama duniani ambayo kitaifa na kimataifa yanaadhimishwa alhamisi ya mwisho ya mwezi aprili kila mwaka .
Amesema kuwa, programu hiyo ilianza mwaka 2016 na mpka kufikia.leo jumla ya watoto wa kike 140 wamenufaika na programu hiyo .
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari ,Nicholaus Merinyo Mkapa ,amesema kuwa wanafunzi wa kike 246 wa shule za sekondari za Umma nchini wameweza kupata mafunzo ya Tehama katika vituo sita vya Zanzibar ,Arusha,Mbeya, Dodoma,Mwanza,na Dar es salaam.
Wamepata mafunzo katika nyanja za matumizi ya teknolojia kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi mafunzo haya yamelenga kuwajengea uwezo ,kuwahamasisha na na kuwapa msukumo wa kujiamini katika kuchagua taaluma ya sayansi ,teknolojia na uhandisi wa hisabati yaani Stemm ,.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “wasichana katika Tehama kwa mabadiliko ya kidigiti jumuishi .,”ikihamasisha ushiriki wa wasichana katika mapinduzi ya kidigitali yanayoendelea duniani .”amesema Mkapa .
Mradi huu umekuwa ukitekelezwa kwa mafanikio makubwa kwa ushirikiano wa UCSAF kama mratibu mkuu ,Costech kama mtoa mafunzo kwa kushirikia na Tamisemi wizara ya Sayansi na Teknolojia ,elimu na mafunzo ya amali Zanzibar na ushirikiano huu ni mfano bora wa namna ya taasisi za umma zinavyoweza kushirikiana juu ya mustakabali wa vijana wetu.
Nao baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo , Jackline Kabogo kutoka Mwadui Technical sekondari amesema kuwa,ameiomba serikali izidi kuwaunga mkono mabinti ili waendeleze bunifu zao mbalimbali ambazo wamezibuni ili ziweze kuwa chachu ya maendeleo katika jamii zetu huku akibainisha kuwa masomo ya Tehama sio ya wavulana peke yao.