Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Aprili 14,2025 amefanya mhadhara na wanafunzi wanaohudhuria Kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam.
IGP Wambura amewakumbusha askari hao kuendelea kutenda kwa usahihi kwa kila hatua ili kutoa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia na kudhibiti uhalifu kwa vitendo.
Amesema, askari Polisi anaowajibu wa kuhakikisha anajenga mahusiano mazuri kati ya jamii na taasisi ili kuweza kubaini, kutanzua na kudhibiti uhalifu na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
Aidha, IGP Wambura, ametumia mhadhara huo kuwakumbusha askari kote nchini kuhakikisha wanasimamia usalama kabla, wakati na baada ya uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

