MTWARA: Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amehitimisha ziara yake katika Mkoa wa Lindi na kupokelewa katika Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuanza ziara yake mkoani humo.
Makalla amewasili na kupokelewa mkoani Mtwara leo Aprili 14,2025 katika Kijiji cha Mpapula na kuelekea katika Ofisi za CCM Mkoa wa Mtwara.
Makalla anatarajiwa kuwa na mkutano wa Hadhara katika Uwanja wa Shule ya Msingi Chikongola Mtwara Mjini.