Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akizungumza jambo wakati akizindua zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na Nchi tisa marafiki ikiwa na lengo la kupambana na matishio ya uharamia ikiwemo usafirishaji harama wa binadamu, silaha pamoja na dawa za kulevya baharini iliyofanyika leo Aprili 13, 2025 katika Bandari ya Dar es Salaam. (PICHA NAOEL RUKANUGA)
Waziri wa Ulinzi Jeshi la Jamhuri ya India Raksha Rajya Mantri akizungumza jambo katika uzinduzi wa zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na Nchi tisa marafiki ikiwa na lengo la kupambana na matishio ya uharamia ikiwemo usafirishaji harama wa binadamu, silaha pamoja na dawa za kulevya baharini.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na Nchi tisa marafiki ikiwa na lengo la kupambana na matishio ya uharamia ikiwemo usafirishaji harama wa binadamu, silaha pamoja na dawa za kulevya.
Picha za matukio mbalimbali katika uzinduzi wa zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na nchi tisa marafiki.
…….
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amezindua zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na Nchi tisa marafiki ikiwa na lengo la kupambana na matishio ya uharamia ikiwemo usafirishaji harama wa binadamu, silaha pamoja na dawa za kulevya baharini yatakayofanyika kuanzia April 13 -18, 2025.
Akizungumza leo April 13, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua zoezi la Afrika India Key Maritime (AIKEYME) ikishirikisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Wanamaji kutoka Jamhuri ya India pamoja na Nchi tisa marafiki Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema kuwa zoezi hilo imelenga kuimarisha ulinzi katika bahari kwani matishio ya usalama yapo mengi.
Mhe. Dkt. Tax amesema kuwa bahari ni kubwa, hivyo ni muhimu kufanya kkwa kushirikiana na Nchi zilizopo mipakani mwa baharini ili inaleta nguvu ya pamoja na kubadilishana mawazo.
“Kunatakuwa na mafunzo pamoja na zoezi, hii ni heshima kwa Tanzania kwani ni mara ya kwanza kufanyika nchini kwetu, haya ni matokeo ya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano na Nchi mbalimbali” amesema Mhe. Dkt. Tax.
Amesema kuwa nchi zote zinazoshiriki zimeleta vifaa pamoja na watu kwa ajili ya kubadilishana mawazo ikiwemo teknolojia ya ulinzi baharini.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, amesema zoezi hilo la pamoja kati ya Tanzania, India pamoja na mataifa tisa ni zoezi la baharini lenye lengo la kukabiliana kwa pamoja na matishio baharini.
“Ni mazoezi ya kawaida kabisa kati ya nchi marafiki ambapo mwaka wa jana tulifanya na nchi ya China na Marekani na mwaka huu tupo na wezetu wa Jeshi la India kwa ajili ya kuweka nguvu ya pamoja na kwa ajili ya kukabiliana na matishio ya baharini” amesema Jenerali Mkunda.
Nae, Waziri wa Ulinzi Jamhuri ya India Raksha Rajya Mantri, amesema kuwa ushirikiano kijeshi wa pamoja ni njia bora ya kujenga uwezo kukabiliana na vitisho vya usalama baharini kususani uharamia, huku akisisitiza kuwa India itaendelea kushirikiana ili kuhakikisha uwepo wa usalama.
Miongoni mwa nchi zinazoshiriki zoezi la pamoja ambazo zinazopakana na bahari ni pamoja na Tanzania, India, Kenya, Afrika Kusini, Djibouti, Msumbiji, Madagascar, Comoro, Shelisheli, Mauritius ambazo zimekuja na meli vita na meli za utawala kwenye mafunzo hayo ya kupambana na matishio baharini.