Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo(IFAD) na wataalam kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025
………
NA. MWANDISHI WETU – DODOMA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Sera,Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha Majumuisho (wrap-up) cha Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Timu ya Wataalamu wanaotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) baada ya kukamilika kwa ziara ya kutembelea na kukagua maeneo yanayotekeleza programu hiyo.
Timu hiyo ya IFAD na wataalam ilitembelea maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa Programu ya AFDP kwa sekta za kilimo na uvuvi Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Aidha, timu hiyo ilitembelea pia Mradi wa Kuimarisha na Kuendeleza Upatikanaji wa Lishe kwa Wafugaji Wadogo wa Viumbe Maji na Wakulima wa Mwani (ARNSA).
Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Aprili, 2025 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma.
Katika kikao hicho Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alipongeza maendeleo mazuri ya utekelezaji program hiyo na kusema kazi zinazofanywa na mradi kwa sasa zinaonekana huku akiwasihi kuendelea kuimarisha mafanikio hayo na kuahidi kushirikiana na TAMISEMI kwa lengo la kuwafikia wanufaika wa program hii.
Baadhi ya wajumbe wakati wa kikao cha majumuisho (Wrap-Up Meeting) kilichohusisha Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na wataalam kutoka katikaSekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Posta Jijini Dodoma Tarehe 11 Aprili 2025
“Serikali kwa kushirikiana na IFAD itahakikisha inaleta matokeo chanya kwa kuzingatia mipango na mikakati inayotekelezwa na Program hii inawanufaisha walengwa,” Akisema Dkt. Yonazi
Aidha, akieleza umuhimu wa Mradi Mkurugenzi Mkaazi wa IFAD Nchini Bw. Sakphouseth Meng amelezea kuwa upo umuhimu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa sehemu ya utekelezaji wa programu ili kuwafikia walengwa na kueleza umuhimu wa sekta binafsi kushirki katika Programu ili kuweza kuwafikia walengwa wengi zaidi na pia kuwa endelevu.