Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania, na Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb), Spika wa Bunge la Tanzania, pia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wakizungumza jambo wakati wakiagana baada ya kikao cha mashauriano kilichofanyika leo Ijumaa, tarehe 11 Aprili 2025, ofisini kwa Balozi Nchimbi, Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma. Pichani kushoto ni Ndugu John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara).
BALOZI NCHIMBI AKUTANA NA MWENYEKITI WA WABUNGE WA CCM, SPIKA WA BUNGE
