Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia historia ya Kiwanda cha kusafisha Mafuta cha Luanda Oil Refinery wakati akihitimisha ziara yake Jijini Luanda nchini Angola tarehe 09 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço wakati akihitimisha ziara yake ya Kiserikali, Luanda nchini Angola tarehe 09 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amehitimisha Ziara yake ya Kiserikali ya siku 3 nchini Angola.
Mapema leo asubuhi, Rais Dkt. Samia alitembelea kiwanda cha kusafisha mafuta cha Luanda Oil Refinery nchini humo.
Mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho, Rais Dkt. Samia amepokelewa na Waziri wa Madini, Mafuta na Gesi wa Jamhuri ya Angola, Mhe.Diamantino Pedro Azevedo ambae alimueleza Rais Dkt. Samia shughuli mbalimbali za kiwandani hapo ikiwemo uzalishaji na teknolojia inayotumika katika uzalishaji kiwandani hapo. Kiwanda cha Oil Refinery kina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Angola ambayo ni nchi ya pili kwa kuwa na hifadhi ya mafuta barani Afrika baada ya Nigeria.
Rais Dkt. Samia amehitimisha ziara yake kwa kuagana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Angola Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço katika Ikulu ya nchi hiyo na kurejea nyumbani Tanzania mapema jioni ya leo.